BREAKING NEWS: Loading latest posts...

Sunday, July 5, 2026

VINARA WA USIMAMIZI WA VIHATARISHI TARURA WAPATIWA MAFUNZO YA MFUMO WA GERMIS


Na Mwandishi Wetu Dodoma


Wakala ya Barabara za Vijijini na Mijini (TARURA) imeandaa mafunzo kuhusu mfumo mpya wa kidigitali wa Usimamizi wa Vihatarishi (GERMIS) kwa Vinara wa Usimamizi wa Vihatarishi wa Wakala huo.

Mafunzo hayo ya siku tano yanatolewa na Mwezeshaji kutoka Ofisi ya Mkaguzi Mkuu wa Ndani wa Serikali, Bi. Adolfina Lugendo yanafanyika katika ofisi ya TARURA ya mradi wa RISE iliyopo katika jengo la PSSSF jijini Dodoma.

Mratibu wa Usimamizi wa Vihatarishi TARURA, Bw. Ally Ismail amesema mfumo wa GERMIS yaani "Government Enterprises Risk Management System" ni mfumo maalum wa kidigitali ulioandaliwa na serikali ili kuhakikisha taasisi zote za serikali zinahama kutoka mfumo wa zamani wa analogia kwenda mfumo wa digitali kwa lengo la kurahisisha usimamizi wake.

Amesema kupitia mafunzo hayo vinara wa Usimamizi wa Vihatarishi TARURA kutoka katika Idara na Vitengo wataweza kuingiza vihatarishi kwenye mfumo ambapo wahusika wa vihatarishi hivyo yaani "Risk Owners" ambao ni Wakuu wa Idara na Vitengo wataweza kuona vihatarishi na udhibiti wake hivyo kuwawezesha kuandaa taarifa zinazotakiwa kwa mujibu wa muongozo wa usimamizi wa vihatarishi.

"Mfumo wa kidigitali wa GERMIS utamuwezesha hata Mtendaji Mkuu ambaye ni Mhusika Mkuu wa Vihatarishi TARURA yaani "Risk Owner" pamoja na Bodi kupata taarifa za vihatarishi kwa wakati ili vile vihatarishi ambavyo vitapelekea kukwamisha majukumu ya TARURA kuweza kuchukuliwa hatua kwa kuwekewa udhibiti ambao utavifanya viwe katika viwango vinavyotakiwa au viwango himilivu yaani "Tolerance Level", amefafanua Bw. Ally Ismail.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages