BREAKING NEWS: Loading latest posts...

Saturday, July 4, 2026

MHE. RIDHIWANI KIKWETE AZINDUA TAFITI SITA ZITAKAZOFANYA TPSC KUWA KITOVU CHA MAARIFA NA USHAHIDI WA KISAYANSI KATIKA KUBORESHA UTUMISHI WA UMMA


Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Ridhiwani Kikwete akibonyeza kitufe wakati akizindua tafiti tumizi sita wakati wa hafla ya kilele cha maadhimisho ya miaka 25 ya Chuo cha Utumishi wa Umma Tanzania (TPSC) zitakazokifanya Chuo hicho kuwa kitovu cha maarifa na ushahidi wa kisayansi kwa ajili ya kuboresha Utumishi wa Umma.


Na. Veronica Mwafisi-Dar es Salaam


Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Ridhiwani Kikwete amezindua tafiti tumizi sita zitakazokifanya Chuo cha Utumishi wa Umma Tanzania (TPSC) kuwa kitovu cha maarifa na ushahidi wa kisayansi kwa ajili ya kuboresha Utumishi wa Umma.

Akizungumza katika hafla ya kilele cha maadhimisho ya miaka 25 ya Chuo cha Utumishi wa Umma Tanzania, Waziri Kikwete amesema Serikali inahitaji tafiti zitakazotoa suluhisho kwa changamoto halisi zinazokabili taasisi za umma.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Ridhiwani Kikwete akizungumza baada ya kuzindua tafiti tumizi sita wakati wa hafla ya kilele cha maadhimisho ya miaka 25 ya Chuo cha Utumishi wa Umma Tanzania (TPSC) yaliyofanyika katika Ukumbi wa Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere kilichopo Jijini Dar es Salaam.




“Tunahitaji tafiti zinatakazosaidia kufanya maamuzi sahihi ya sera, kuboresha mifumo ya kazi, na kuongeza ufanisi wa huduma kwa wananchi, amesema Mhe. Kikwete.

Aidha, Waziri Kikwete amewapongeza watafiti wote walioshiriki katika kazi ya utafiti na kutoa rai kwa Chuo cha Utumishi wa Umma Tanzania kuendelea kuimarisha ushirikiano na Wizara, Idara Zinazojitegemea, Wakala za Serikali, Mamlaka za Serikali za Mitaa, Vyuo Vikuu na taasisi nyingine ili tafiti zake ziwe na mchango mkubwa katika maendeleo ya Taifa.

Waziri Kikwete ameongeza kuwa, anaamini miaka 25 ijayo itakuwa kipindi cha mafanikio makubwa zaidi, ambapo Chuo hicho kitaendelea kuwa kinara wa maendeleo ya rasilimali watu, tafiti tumizi, na ushauri wa kitaalamu kwa ajili ya kuimarisha Utumishi wa Umma na kuchochea utekelezaji wa Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050.






No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages